IQNA

Hafla ya kumuenzi Ibn Sina (Avicenna) yafanyika Hamedan, Iran

TEHRAN (IQNA) Kumefanyika hafla ya kumunezi kumuenzi Hassan bin Abdullah maarufu kwa jina la Abu Ali bin Sina (Avicenna) ambayo inatambuliwa kuwa ni Siku ya Daktari nchini Iran.

Hafla hiyo imefanyika katika mji wa Hamedan alikozikwa msomi huyo maarufu. Kila mwaka tarehe Mosi Shahrivar iliyosadifiana na Agosti 23 nchini Iran inatambuliwa kuwa ni Siku ya Daktari nchini Iran kama njia ya kumuenzi Ibn Sina.

Ibn Sina mwanafalsafa na tabibu mashuhuri wa Kiislamu na Kiirani aliyejulikana pia kwa laqabu ya Sheikhul Rais alizaliwa tarehe 3 Safar mwaka 370 Hijria Qamaria katika mji wa Balkh. Ibn Sina alihifadhi Qur'ani yote alipokuwa na umri wa miaka 10. Msomi na tatibu huyo mashuhuri wa Kiislamu alijifunza tiba baada ya kupata elimu za mantiki, hisabati, nujumu, falsafa pamoja na elimu nyinginezo. Alianza kuandika vitabu akiwa na umri wa miaka 21 na miongoni mwa vitabu vyake maarufu ni Qanun, Shifaa na Isharaat.