IQNA

Usomaji Qur'ani wa mtoto wa Kimisri Kongamano la Dini nchini Bahrain (+Video)

TEHRAN (IQNA) – Kongamano la mazungumzo ya dini mbalimbali lilifanyika nchini Bahrain mapema mwezi huu na lilihudhuriwa na Kiongozi wa Kanisa Katoloki Papa Francis na Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu Al-Azhar cha Misri Sheikh Ahmed el-Tayeb.

Kongamano lilifunguliwa kwa usomaji wa Qur'ani Tukufu na qari mdogo sana kutoka Misri.

Omar Ali, ambaye ni miongoni mwa wasomaji Qur'ani kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar, alisoma aya ya 33-36 ya Surah Yasin:

“Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila!  Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake. Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua. ”

Picha zifuatazo zinaangazia usomaji wake kwenye mkutano huo:

Kishikizo: omar ali ، qarii ، misri ، papa francis ، al azhar