IQNA – Gavana wa Dakahlia, nchini Misri, amemtunuku nakala ya Qur’ani Tukufu Imam Ashour, mchezaji wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Al-Ahly, ikiwa ni ishara ya kutambua juhudi zake katika Kombe la Dunia la mwaka 2026.
Habari ID: 3482508 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19
IQNA – Programu ya ‘Noor’, inayorushwa kupitia Kituo cha Televisheni cha Naas nchini Misri, iliwasilisha ujumbe wa elimu na malezi kwa mtindo rahisi kwa ajili ya watoto katika kipindi chake kipya siku ya Ijumaa.
Habari ID: 3482507 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19
IQNA – Msururu wa usomaji wa Qur’ani wenye kuvutia ambao uliwapagawisha majaji na hadhira kwa pamoja umeshuhudiwa katika raundi za awali za msimu wa pili wa shindano la “Dawlet El-Tilawa” (Dola ya Usomaji) nchini Misri. Tukio hili linadhihirisha kipaji cha kipekee na juhudi za hali ya juu za washiriki kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo katika kulihudumia Kitabu Kitukufu.
Habari ID: 3482503 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/18
IQNA – Maktaba ya Alexandria imeandaa kongamano lililopewa anuani ya: “Usomaji wa Qur’ani nchini Misri; Utafiti wa Ukuzaji na Kuporomoka Kwake,” ikiwa ni sehemu ya programu ya kiutamaduni katika Maonesho ya Vitabu ya Kimataifa ya maktaba hiyo.
Habari ID: 3482485 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14
IQNA – Idara ya Taasisi za Kituo cha Kiislamu cha Al‑Azhar imeanzisha mpango wa kugawa nakala za Qur’ani Tukufu kwa Maktab (vituo vya jadi vya kuhifadhi Qur’ani) kote nchini Misri.
Habari ID: 3482390 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/22
IQNA – Wiki hii imeadhimisha kumbukumbu ya kuaga dunia kwa mmoja wa mabingwa wakubwa wa madrasah ya Misri katika sanaa ya usomaji wa Qur’ani, Sheikh Mohammad Siddiq Al‑Minshawi. Tukio hili linawakumbusha Waislamu kuhusu qiraa yake ya kina na yenye ikhlasi ambayo hadi leo inaendelea kusikika na kugusa nyoyo katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3482385 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/21
IQNA – Wizara ya Awqaf ya Misri imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa marehemu Sheikh Mustafa Ismail, mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur’ani nchini humo.
Habari ID: 3482384 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/21
IQNA – Baba na mwanae kutoka Misri waliokuwa washiriki katika Tuzo ya Qur’ani ya Al Ameed nchini Iraq wamekuwa miongoni mwa waliopata nafasi za juu katika shindano hilo la kimataifa la usomaji wa Qur’ani.
Habari ID: 3482368 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/16
IQNA – Kisa hiki kinaanza katika miaka ya 1960, pale Sheikh Mohamed Siddiq Al‑Minshawi aliporekodi usomaji wa Qur’ani Tukufu yote kwa ajili ya Redio au Idhaa ya Qur’ani ya Misri.
Habari ID: 3482359 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/14
IQNA – Idhaa ya Qur’ani ya Misri kila siku katika kipindi chake cha jioni hurusha tilawa za Ibrahim Shasha’i, mwana wa qari mashuhuri wa Kimisri marehemu Sheikh Abdel Fattah Shasha’i.
Habari ID: 3482346 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/10
IQNA – Mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Misri ya mwaka huu yatafanyika kwa kumbukumbu ya qari mashuhuri marehemu Sheikh Abdel Fattah Shaasha’i.
Habari ID: 3482326 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/05
IQNA – Idhaa ya Qur’ani Tukufu ya Misri, yenye makao yake Cairo, imeanza kurusha hewani usomaji wa Qur’ani kwa mtindo wa tarteel wa miaka ya 1960 wa qari mashuhuri Sheikh Mohamed Siddiq El‑Minshawi.
Habari ID: 3482318 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/03
IQNA – Chuo cha Kimataifa cha Al-Azhar nchini Misri kiliandaa programu ya ziara ya maimamu, wahubiri na walinganiaji wageni kutembelea vivutio vya kihistoria vya Kiislamu na Kikristo katika eneo la Fustat.
Habari ID: 3482315 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/02
IQNA – Wengi wanaamini kuwa kurekodiwa kwa Surat Yusuf kulikuwa mgeuko wa kweli katika maisha ya Sheikh al-Sayyid Saeed, na mafanikio hayo makubwa yakamfanya ajipatie umaarufu na hatimaye kunyakua lakabu inayostahiki ya “Sultan al-Qurra” (Mfalme wa Wasomaji Qur’ani).
Habari ID: 3482308 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/31
IQNA – Kijana mdogo kutoka nchini Misri amewastaajabisha waandaaji wa programu ya Siku ya Qur’ani nchini Oman, baada ya kufanikiwa kusoma Qur'ani Tukufu nzima kwa kichwa (hifdhu) ndani ya muda wa saa nane pekee, akionyesha ustadi wa hali ya juu na weledi wa kustaajabisha.
Habari ID: 3482280 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/25
IQNA – Ofisi ya Amal ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu imezinduliwa rasmi katika hafla maalumu iliyoandaliwa katika Mkoa wa Sinai, nchini Misri.
Habari ID: 3482239 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/15
CAIRO – Vikosi vya usalama jijini Cairo, Misri, vimefunga duka la vitabu lililokuwa linafanya kazi bila kibali katika eneo la Darb al‑Ahmar baada ya kubainika kuwa lilikuwa likisambaza na kuuza nakala za Qur’ani Tukufu (Misahafu) bila kupata vibali vinavyotakiwa kisheria.
Habari ID: 3482234 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/13
IQNA – Wizara ya Awqaf ya Misri imetangaza uungaji mkono wake kamili kwa vituo vya kuhifadhi Qur’ani Tukufu pamoja na kuendeleza programu zake za kielimu na kimaadili.
Habari ID: 3482225 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/11
IQNA – Sheikh Muhammad Mahmoud Tablawi, mmoja wa maqari mashuhuri na wenye taswira ya kipekee nchini Misri, alifariki dunia miaka sita iliyopita baada ya kutumikia Qur'ani Tukufu kwa zaidi ya miaka sitini.
Habari ID: 3482220 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/09
IQNA – Sheikh Muhammad Abdulaziz Hissan, qari mashuhuri wa Misri aliyekuwa na ulemavu wa macho, alikuwa na shule ya kipekee ya sauti na maqam, na aliacha nyuma mamia ya kanda za usomaji wa Qur’ani Tukufu ambazo bado zinatangazwa na vyombo vya habari vya Misri na nje ya Misri.
Habari ID: 3482202 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/05