IQNA

Baba na mwanawe Misri Wanasoma Qur'ani kwa Pamoja (+Video)

TEHRAN (IQNA) - Baba na mwanawe nchini Misri hivi karibuni wamesambaza klipu za usomaji wao wa pamoja wa Qur'ani kwenye mitandao ya kijamii.

Katika klipu, wawili hao wanasoma aya ya kwanza hadi ya tisa ya Surah Al-Fajr (89):

"Naapa kwa alfajiri. Na kwa masiku kumi. Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja. Na kwa usiku unapo pita. Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?  Wa Iram, wenye majumba marefu?  Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?"