IQNA

Mtoto wa Syria anasoma aya za Qur'ani pembizoni mwa Mashindano ya Qur'ani nchini Kuwait +Video

TEHRAN (IQNA) – Klipu ya video imesambazwa mtandaoni ikimuonyesha mtoto Msyria akisoma Qur'ani Tukufu kwa Tartil. Jafar Faras al-Hibal, ambaye ana umri wa miaka kumi, alisoma pembizoni mwa mashindano ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani ya Kuwait.

Alikuwa mshindani katika mashindano hayo ya  Qur'ani lakini usomaji huu haukufanyika kama sehemu ya mashindano.
Jafar alisoma aya hizo katika banda la Jumuiya ya Kuhifadhi na Kufundisha Qur'ani ya Abi Shuaib al-Dakali katika maonyesho yaliyowekwa kando ya mashindano hayo.
Katika klipu hii, qari mchanga anasema Sura za Al-Fatiha, Al-Fil na Quraish za Qur'ani Tukufu.


4145035