IQNA

Qari wa Bangladesh akisoma aya za Surah Hud (+Video)

DHAKA (IQNA) – Qari wa Bangladesh Saidul Islam Asad hivi majuzi alikariri aya za Surah Hud, ambazo picha zake zimetolewa mtandaoni. Katika picha hii, asoma aya za Sura ya 41 na 42.

Na akasema: "Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri."