IQNA

Qari kijana Mmisri akisoma aya za Sura Al-Qasas katika Qur’ani Tukufu (+Video)

CAIRO (IQNA) – Abdul Razzaq al-Shihawi ni qari kijana kutoka Misri ambaye hivi karibuni amepata umaarufu kwa usomaji wake mzuri wa Qur’ani Tukufu.

Hivi majuzi, klipu ya  usomaji wake wa aya za Sura Al-Qasas imesambaa katika mitandao ya kijamii.

Katika video hii, anakariri Aya ya 7 hadi 9 ya Sura Al Qasas:

 Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.  Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa. Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua.

Qiraa hii ilikuwa  mbele ya jopo la majaji wa Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani ya Katara nchini Qatar.