IQNA

Qari Maarufu wa Iran akisoma aya za Surah Al-Insan katika kumbukumbu ya Bibi Fatima (SA)

IQNA – Qari mashuhuri wa Iran Mohammad Reza Purzargari amesema aya ya 5-18 ya Surah Al-Insan katika hafla iliyofanyika wiki iliyopita ya kuadhimisha kumbukumbu ya kufa shahidi Bibi Fatima Zahra (SA) mjini Tehran katika ukumbi wa kidini wa Husseiniya ya Imam Khomeini (MA)

Hapa chini ni tarjama ya aya hizo

5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri, 


6. Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. 


7. Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,


8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. 


9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. 


10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. 


11. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha. 


12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. 


13 Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. 


14 Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. 


15 Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae, 


16 Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. 


17 Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi. 


18 Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.