IQNA

Msikiti wa Jamkaran wapambwa kabla ya Idi ya Nisf Sha'ban

Msikiti wa Jamkaran ulio katika mji wa Qom nchini Iran umepambwa kwa mataa ili kuutayarisha kwa ajili ya sherehe za siku ya katikati ya Sha’aban ambayo pia ni maarufu kama Nisf Sha'ban.
Nisf Sha'ban , au siku ya 15 ya mwezi wa Hijria Qamari wa Sha’aban, ni siku ya  kuzaliwa Imam Mahdi, ambaye ni Imamu wa kumi na mbili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia ambaye pia anajulikana kama Imam Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake). Kila mwaka katika hafla hii adhimu, Msikiti wa Jamkaran hutembelewa na mamia ya maelfu ya waumini. Siku ya 15 ya Sha’aban inasadifiana na Jumatano, Februari 25, mwaka huu.