IQNA

Qiraa

Qari Ahmadivafa wa Iran akisema Qur'ani Tukufu katika hafla ya kuapishwa rais mpya wa Iran

IQNA - Hamid Reza Ahmadivafa ndiye qari aliyechaguliwa kusoma Qur'ani Tukufu kufungua hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Iran Daktari Masoud Pezeshkian 30 Julai 2024.

Sherehe hizo zilifanyika katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) mjini Tehran na kuhudhuriwa maafisa wa serikali,  wabunge pamoja na viongozi wa ngazi za juu kutoka zaidi ya nchi 88.

Qari huyu  mashuhuri wa Iran Ahmadivafa alisoma ya Aya za 89-91 ya Surah An-Nahl

Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.

Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo.

4229140

 

Kishikizo: qari ، iran