Alisoma aya za Surah An-Nasr katika Qur'ani Tukufu
“Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu"
Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,
Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,
Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.
Qari Moslemi alizaliwa mwaka 1998, na alianza kujifunza Qur'ani akiwa na umri wa miaka 3 katika mji aliozaliwa wa Qaemshahr, kaskazini mwa Iran, kwa kuungwa mkono na wazazi wake, na amekuwa qari maarufu katika miaka ya hivi karibuni.
4243491