IQNA

Qari: Kipindi cha Qur’ani cha Iran “Mahfel” chavuma kimataifa

15:25 - September 21, 2025
Habari ID: 3481263
IQNA –Qari na Mtangazaji wa kipindi maarufu cha Qur’ani cha televisheni ya Iran, Mahfel, amesema kuwa kipindi hicho kimepata umaarufu mkubwa kimataifa, kikivutia watazamaji kutoka ulimwengu wa Kiislamu na hata katika maengine ya dunaini.

“Leo hii, ni wachache tu katika nchi za Kiislamu—na hata baadhi ya zisizo za Kiislamu—ambao hawajawahi kusikia kuhusu Mahfel,” alisema Ahmad Abulqasemi, qari mashuhuri wa kimataifa kutoka Iran, katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA). “Athari za kipindi hiki ni dhahiri na wa kushikika, kiasi kwamba huhitaji maelezo marefu. Tunayaona waziwazi katika safari za nje na mawasiliano na jumuiya za Qur’ani.”

Mahfel huonesha usomaji wa Qur’ani na hufundisha maadili ya Kiislamu, na ni miongoni mwa vipindi vinavyothaminiwa sana duniani. Hurushwa kila siku kabla ya Magharibi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kupitia chaneli ya TV 3 ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), na huwapa watazamaji pumziko la kiroho wanapojiandaa kufuturu.

Lengo kuu la kipindi hiki ni kuimarisha nyakati fupi za utulivu kwa wanaofunga kupitia mijadala yenye maarifa na usomaji wa kuvutia wa Qur’ani Tukufu.

Qari Abulqasemi alisisitiza upeo wa kipindi hicho katika maeneo mbalimbali: “Katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Tanzania yenye historia ya Qur’ani, jumuiya za kidini zinafahamu Mahfel vyema. Hali hii haijabakia Afrika pekee; katika nchi zenye Waislamu wengi kama Pakistan na Bangladesh, kipindi hiki kina watazamaji wengi.”

Alikadiria idadi ya watazamaji: “Kwa ujasiri tunaweza kusema kuwa asilimia 80 hadi 90 ya nchi za Kiislamu zimewahi kutazama Mahfel. Kwa idadi ya watu, watazamaji wa nje ya Iran si wachache kuliko wa ndani.”

Iranian Quranic Program Mahfel Gains Widespread Int’l Viewership, Host Says

Qari Abulqasemi

Alisimulia visa vya kuvutia kuthibitisha umaarufu wa Mahfel: “Huko Afghanistan, hata maafisa wa uwanja wa ndege walitutambua na kuturuhusu kuingia bila taratibu rasmi. Na katika uwanja wa ndege wa Kenya, nchi isiyo ya Kiislamu, mhudumu wa mizigo alitutambua kwa furaha na akakumbuka Mahfel. Visa kama hivi vinaonesha hadhi ya kimataifa ya kipindi hiki.”

Qari Abulqasemi alihusisha mafanikio ya Mahfel na vipengele viwili: vipaji vya wasomaji wa Iran na kampeni ya kimkakati ya vyombo vya habari vya kidijitali. “Mahfel sasa ni chombo kikuu cha Qur’ani katika vyombo vya habari. Mafanikio haya yanatokana na mvuto wa shughuli za Qur’ani na vipaji vya kipekee vya wasomaji wa Iran, pamoja na juhudi za timu ya vyombo vya habari waliotafsiri kipindi hiki kwa lugha tano na kukisambaza kupitia mitandao ya kimataifa kama YouTube.”

Kwa mujibu wa mkakati huo, alitoa takwimu maalum: “Zaidi ya watu milioni 100 nje ya Iran wameangalia Mahfel. Hili ni jambo la kipekee kwa kipindi cha Qur’ani.”

Qari Abulqasemi pia alieleza kuwa kipindi hicho kinabadilisha mtazamo wa kimataifa kuhusu Iran: “Zamani, baadhi ya watu walidhani kuwa Wairani hawana uelewa wa Qur’ani. Lakini kupitia vipindi kama hivi, dhana hizo zimebadilika. Popote ambapo msomaji wa Qur’ani kutoka Iran amesoma, watu wamegundua kuwa taifa hilo haliwezi kuwa mbali na Qur’ani.”

Alihitimisha kwa kusema: “Leo hii, Qur’ani inaweza kujibu mahitaji mengi ya ulimwengu wa Kiislamu. Imani ambayo mataifa mengine sasa wanayo kwa Wairani ni matokeo ya vipindi kama Mahfel. Hii ni mwanzo tu wa safari, na matunda yake makubwa bado yanakuja. Rasilimali watu hawa wa Qur’ani ndio mafanikio makubwa ya Mahfel. Kwa uwepo wao, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mustakabali wa jamii ya Qur’ani ya Iran ni wenye nuru.”

3494681

Habari zinazohusiana
captcha