IQNA

Qiraa ya Peponi

Qiraa ya Peponi: Msikilize Qari Al Banna akisoma aya za Sura Ta-Ha

IQNA – Ifuatayo ni sehemu ya qiraa ya marehemu qari wa Misri, Mahmud Ali Al-Banna, akisoma aya ya 114 ya Surah Ta-Ha.

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema wakati mmoja kwamba kuisikiliza Qur'an humfanya mja kupokea thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, huku kila herufi ikisikika huhesabiwa kuwa ni amali njema kwa msikilizaji, na kumpandisha hadi kufikia daraja wale wanaosoma Qur'ani Tukufu na kupaa kuelekea peponi.

Kuzama katika aya za Qur'ani Tukufu ambazo zina mvuto wa aina yake wa kimaanawi  humfanya  msikilizaji kuwa katika duara la huruma ya Mwenyezi Mungu.

IQNA imeandaa mfululizo wa qiraa za Qur'ani Tukufu  ujulikanao kama " Qiraa ya Peponi,"  ambapo katika mfululizo huu kuna visomo vya maqarii maarufu wa Qur'ani Tukufu duniani.