Bendera ya Haram ya Imam Ridha (AS) yabadilishwa kuashiria kumalizika maombolezo ya Muharram na Safar
IQNA - Katika hafla ya Septemba 7, 2024, bendera nyeusi juu ya kaburi la Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazni mashariki mwa Iran ilibadilishwa na ile ya kijani. Mabadiliko ya bendera yanakuja wakati siku za maombolezo katika miezi ya mwandamo ya Muharram na Safar imefika ukingoni kwa kuwadia Rabi' al-Awwal, mwezi wa kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW)