IQNA

Mawkib zahudumia wafanyaziara katika Msikiti wa Jamkaran wakati wa sherehe za Nisf Shaaban

IQNA – Takriban mawkiba 500 zimetoa huduma mbalimbali kwa mamia ya maelfu ya wafanyaziara ambao waliokuwa wakisherehekea sherehe za Nisf Shaaban katika Msikiti wa Jamkaran huko Qom. (Picha zilipigwa Februari 13, 2025)

Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) na kupata sehemu ya kupumzika.