Tamasha la Kimataifa la Iftar (futari) laleta pamoja wanafunzi kutoka mataifa 40 jijini Tehran
IQNA – Jiji la Tehran Tehran limekuwa mwenyeji wa tamasha la pili la "Futari ya Kimataifa," lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Ahlul Bayt (AS).
Wanafunzi wa kimataifa kutoka kote Iran walishiriki, wakitayarisha vyakula vya kitamaduni ambavyo hutumika Mwezi wa Ramadhani katika nchi zao katika tamasha hilo, lililofanyika Machi 9, 2025.
Wageni mashuhuri, wakiwemo maafisa wa serikali, mabalozi, na wasomi, walihudhuria tukio hilo, ambalo lililenga kuhamasisha mabadilishano ya kitamaduni na umoja kupitia desturi ya pamoja ya iftar.