IQNA

Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait AS, Tehran

Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait AS umeanza Jumamosi mjini Tehran kwa hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mkutano huo unahudhuriwa na wageni 500 waalikwa kutoka nchi 130 duniani. Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait AS ilianzishwa 1990 na vikao vya baraza kuu lake hufanyika mara moja kila miaka minne.