IQNA

Maandamano yaendelea Jordan na Palestina kupinga muamala wa karne

Wananchi wa Jordan na Palestina, Ijumaa 21 Februari 2020 waliandamana kwa Ijumaa ya nne mfululizo kupinga ule mpango wa 'muamala wa karne' wa Rais Donald Trump kuhusu kadhia ya Palestina. Nchini Jordan wananchi wameandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Amman.