IQNA

Taa ya Ramadhani, utamaduni wa kale Palestina

Wakati wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Wapalestina hununia na kuwasha taa maalumu kwa lengo la kusherehekea mwezi huu mtukufu.

Vizazi kwa vizazi vimekuwa vikipokezana utamaduni huu ambao huhuishwa katika miji mbali mbali ya Palestina, ikiwemo sehemu kongwe ya Mji wa Quds (Jerusalem). Taa hizi huwa kubwa na ndogo zikiwa na anuai ya mapambo na nakshi za rangi mbali mbali na muhimu zaidi ni maandishi aya za Qur’ani Tukufu