Corona ni fursa kwa mazingira ya dunia kuweza 'kupumua'
Ingawa janga la COVID-19 au corona limesababisha hasara katika sekta mbali mbali dunaini hasa kutokana na kufungwa biasahra, masomo na utalii n.k. lakini janga hili limekuwa ni fursa kwa mazingira kupata uhai mpya. Kupunguzwa kabisa shughuli za kiviwanda, usafiri uwe ni wa nchi kavu, angani na baharini kumepelekea mazingira kutochafuliwa. Miji mingi duniani imekuwa ikisumbuliwa na uchafuzi wa mazingira lakini sasa baada ya janga la COVID-19 mazingira yamepata uhai mpya kutokana na kupungua au kusitishwa shughuli haribifu za mwanadamu