IQNA

Msikiti wa Dimaukom , nembo ya jamii kuishi kwa maelewano nchini Ufilipino

TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Dimaukom , katika mkoa wa Maguindanao eneo la Datu Saudi Ampatuan,ni moja kati ya vivutio vya utalii nchini Ufilipino.

Msikiti huo ulifunguliwa mwaka 2014 na kuta zake zina rangi ya waridi ambayo ni nembo ya amani na sasa ni kivutio cha utalii kutokana na usanivu majengo wake na nguzo ya maelewano baina ya wafuasi wa dini mbali mbali.