Leo ni Jumapili tarehe 25 Rajab 1443 Hijria sawa na Februari 27 mwaka 2022. Siku kama ya leo miaka 1260 iliyopita, Imam Musa Kadhim AS mmoja wa wajukuu watoharifu wa Mtume Muhammad SAW aliuawa shahidi. Imam Kadhim SAW alizaliwa mwaka 128 Hijiria huko katika eneo la Ab'waa lililoko baina ya miji mitakatifu ya Madina na Makka.