IQNA

Mandhari ya kuvutia ya Msikiti wa kihistoria wa Masjid Jamia, Qom

TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Jamia katika mji mtakatifu wa Qom, Iran, ni moja ya misikiti mikongwe zaidi nchini. Ingawa hakuna chuma kilichotumika katika ujenzi wa msikiti huu wenye mandhari ya kuvutia na kuba yake, bado umesimama kwa nguvu baada ya karne nyingi.

Msikiti huo wenye ukubwa wa mita za mraba 6,000 ulijengwa katika karne ya 3 Hijria na Abulsadim Ash’ari, ambaye alikuwa sahaba wa Imam Hadi (AS) na Imam Hassan Askari (AS).

.