IQNA

Siku ya 5 ya Mashindano ya 63 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia

KUALA LUMPUR (IQNA) –Mashindano ya 63 ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysiaa yaliendelea Jumatano ambayo ilikuwa siku ya tano na ya mwisho katika kategoria za kuhifadhi na kusoma.

Jumla ya wawakilishi 76 kutoka nchi 52 wamepangwa kushindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani. Kwa mujibu wa taarufa, wanaume 24 na wanawake 12 wanashindana katika kitengo cha usomaji ambacho kinafanyika jioni, na wanaume 27 na wanawake 13 katika kitengo cha kuhifadhi  kinafanyika  asubuhi.

Matukio yote ya mashindano hayo yanaonyeshwa moja kwa moja kutoka kwa akaunti za mitandao ya kijamii za Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM). Mashindano hayo yatakamilika Agosti 24.