IQNA

Klipu mbili fupi za usomaji Qur'ani Tukufu wa Ustah Mahmoud Shahat Anwar

Klipu mbili za qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Ustadh Mahmoud Shahat Anwar akisoma Sura Al Kahf mwaka wa 2008 na 2023 zimesambazwa mtandaoni.

Katika klipu hizi Ustadh Mahmoud Shahat Anwar anasema Aya ya 21 ya Surah Kahf, “Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao." Qiraa hii ni ya mtindo wa Ajam. 

 

Ustadh Shahat Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1979. Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Iraq, Iran, Qatar, UAE, Algeria, Syria, Pakistan, Afrika Kusini, Ugiriki, Uturuki na Ubelgiji.