IQNA

Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina na kulaani utawala katili wa Israel yaendelea duniani

Maandamano ya kupinga kuendelea mauaji ya kikatili yanayofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza yanaendelea katika nchi mbalimbali za dunia. Wananchi wa nchi hizo wamelaani mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina yanayotekelezwa na utawala katili wa Israel kwa kushika bendera za Palestina na kushikilia wanasesere kuwakumbuka watoto wa Ghaza.

Maandamano ya hayo yanafnayika huku idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi hadi sasa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ikipindukia 10,000 ambapo wengi ni wanawake na watoto wadogo.