Miaka 35 iliyopita, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (MA) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 87. Ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na majonzi na huzuni kubwa kuutokana na kutangazwa kifo cha Imam. Alianza kujishughulisha na siasa sambamba na masuala ya kielimu na kiutamaduni. Mapambano ya Imam dhidi ya utawala wa Shah na uingiliaji wa Marekani nchini Iran yalishtadi mwaka 1963 na kupelekea Imam kubaidishwa kwa miaka 13 nchini Iraq, Uturuki na Ufaransa. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi shupavu wa Imam Khomeini (MA).