IQNA - Hauli ya mwaka wa 35 tokea alipoaga dunia Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu), muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanyika katika mji mtakatifu wa Madina wiki hii.
Hujjatul Islam Abdul Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya Hija alihutubia hadhirina katika hauli hiyo.