IQNA

Kisomo cha Mbinguni: Sayyid Metwaly Abdel Aal akisoma Surah Al-Hashr

IQNA – Ifuatayo ni sehemu ya qiraa ya marehemu qari wa Misri, Sayyid Metwaly Abdel Aal, akisoma aya ya 23-24 ya Surah Al-Hashr katika Qur'ani Tukufu

Mtume Muhammad (SAW) alisema wakati mmoja kwamba kuisikiliza Qur'ani Tukufu kunapata thawabu za Mwenyezi Mungu, huku kila herufi ikisikika ikistahiki tendo jema kwa msikilizaji, na kumpandisha msikilizaji safu ya wale wanaosoma maandiko matukufu na kupaa kuelekea mbinguni. 

Shirika la habari la IQNA limeratibu na kutoa mfululizo unaoitwa "Kisomo cha Mbinguni," yenye kumbukumbu za kuvutia za wasomaji maarufu Qur’ani Tukufu.