Majeruhi wa Lebanon wa Mashambulizi ya Pager ya Israel watembelea Haram ya Imam Ridha (AS)
IQNA - Kundi la raia wa Lebanon na wapiganaji wa Hizbullah, ambao walijeruhiwa katika shambulio la hivi karibuni la kigaidi la Israel dhidi yao walitembelea Haram ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad mapema Oktoba 2024.
Idadi ya watu waliojeruhiwa walihamishiwa Iran kwa matibabu kufuatia shambulio la Israel mnamo Septemba 17.