IQNA – Nyumba ya Kihistoria ya Tabatabaei iliyoko katika mji wa Kashan, katikati mwa Iran, ni mojawapo ya majengo maarufu zaidi ya enzi ya kipindi cha Qajar.
Ilijengwa katika miaka ya 1880 na mfanyabiashara maarufu na tajiri wa wakati huo aliyeitwa Sayyid Jafar Tabatabaei. Nyumba hiyo ina ukubwa wa mita za mraba 4,730 na ilichukua takriban miaka 10 kukamilika kujengwa.