IQNA

Usomaji wa Aya za Surah al-Fath kwa Tartili na Qari Kutoka Ivory Coast

IQNA – Baladi Omar, qari mashuhuri wa Qur’ani kutoka nchi ya Ivory Coast ya Afrika Magharibi, ameshiriki katika kampeni ya Qur’ani ya “Fath” kwa kusoma aya nne za mwanzo kutoka Surah al-Fath kwa tartili.

Kwa mujibu wa ripoti ya IQNA, Baladi Omar, ambaye ni qari na hafidh maarufu kutoka Ivory Coast, alishiriki katika kampeni ya Qur’ani ya “Fath” kwa usomaji wa aya za mwanzo za surah hiyo tukufu.

Kampeni hii ya Qur’ani iitwayo “Fath” ilizinduliwa na Shirika la Habari la Kimataifa la Qur’ani (IQNA) kufuatia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika hali ambapo maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu wanajaribu kueneza hofu na kukatisha tamaa miongoni mwa wananchi wa Iran kwa njama mbalimbali.

Lengo la kampeni hii ni kuimarisha moyo wa matumaini na imani miongoni mwa Waislamu kupitia ujumbe wa Qur’ani Tukufu, hasa katika nyakati za mitihani na majaribu.

 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 


1. Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri 

2. Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyo tangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika Njia Iliyo Nyooka, 

3. Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu 
4. Yeye ndiye aliye teremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima 
4294204
Kishikizo: ivory coast ، qurani tukufu