IQNA

Usomaji wa Pamoja wa Surah Al-Balad na Maqari Wavulana

IQNA – Video mpya imezinduliwa ikionyesha usomaji wa pamoja wa Surah Al-Balad kutoka kwa vijana wa kikundi cha Tasnim Tawasheeh
Usomaji huu umetungwa kwa msukumo wa qiraa’ maarufu ya Qari mashuhuri wa Misri marehemu Sheikh Abdul Basit Abdul-Samad (Rahimahullah). Mandhari ya video hii yanaonesha kwa ubunifu uzuri wa kihistoria wa Msikiti wa Nasir al-Mulk ulioko Shiraz, Iran.
 
Ifuatayo ni tafsiri ya Surah Al-Balad kwa Kiswahili:
Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
1.  Naapa kwa Mji huu!  
2.  Nawe unaukaa Mji huu.  
3.  Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.  
4.  Hakika tumemuumba mtu katika taabu.  
5.  Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?  
6.  Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.  
7.  Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?  
8.  Kwani hatukumpa macho mawili?  
9.  Na ulimi, na midomo miwili?  
10. Na tukambainishia zote njia mbili?  
11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.  
12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?  
13. Kumkomboa mtumwa;  
14. Au kumlisha siku ya njaa  
15. Yatima aliye jamaa,  
16. Au masikini aliye vumbini.  
17. Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.  
18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.  
19. Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.  
20. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.

3493748

Kishikizo: qiraa