IQNA

Waislamu na Wakristo waungane kupinga jinai za Israel huko Gaza

10:23 - December 30, 2008
Habari ID: 1724738
Kiongozi mwandamizi wa Waislamu wa Kishia nchini Lebanon Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah ametoa wito kwa Waislamu na Wakristo kuwa na msimamo wa pamoja katika kutetea taifa linalodhulumiwa la Palestina.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Lebanononline, katika ujumbe wake kwa Walebanoni, Waarabu, Waisalmu na Wakristo kwa mnasaba wa kuzaliwa Nabi Issa AS na kuanza mwaka mpya wa Hijria Qamariya na ziku za maombolezo za Ashura, Allamah Fadhlullah ametangaza kuwa, ‘Waarabu na Waislamu wanapaswa kutangaza uungaji mkono wao wa kibinadamu kwa watu wasio na hatia wa Palestina, Iraq, Afghanistan, Sudan na Somalia’. Ameendelea kusema kuwa, Waislamu na Wakristo wanapaswa kuonyesha uadui wao kwa vikosi vya maadui na maghasibu.
Mwanachuoni huyo mwandamizi wa Lebanon amesisitiza kuwa, hali ya kusikitisha iliyopo hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu haitokani tu na hujuma ya madola yenye kiburi na kukaliwa kwa mabavu nchi hizo bali pia inatokana na udhaifu wa ndani ya nchi hizo.
Marjaa huyo wa Kishia wa Lebanon ameongeza kuwa, katika kulipiza kisasi dhidi ya harakati za mapambano na intifadha, hivi sasa baadhi ya duru rasmi za Kiarabu zinafanya mazungumzo ya wazi na adui kwa malengo ambayo yameshajulikana.
Allamah Fadhlullah amemaliza kwa kuashiria hali ya hivi sasa nchini Lebanon na kusema, ‘Lebanon inapitia kipindi ambacho inahitajia umoja wa wakazi wake. Hii ni kwa sababu makundi ya kieneo na kimataifa yanataka kuwa na satua katika nchi hiyo ndogo’. 340080
captcha