IQNA

Wakenya 6,000 kushiriki katika Ibada ya Hija

9:06 - April 04, 2017
Habari ID: 3470917
TEHRAN (IQNA)-Raia 6,000 wa Kenya wanatazamiwa kushiriki katika Ibada ya Hija mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, serikali ya Saudi Arabia imeongeza idadi ya Waislamu Wakenya wanaoruhusiwa kuhiji kutoka elfu nne hadi elfu sita. Iwapo nafasi hizo zote zitatumiwa, hiyo itakuwa idadi kubwa zaidi ya Wakenya kuwahi kutekeleza ibada ya Hija.

Kufuatia ongezeko la idadi ya Wakenya wanaoweza kuhiji, tayari mipango ya awali kwa ajili ya safari ya Hija imeshaanza ili kufanikisha zoezi la kuwatuma mahujaji.

Naibu Mkuu wa Idara ya Hija Kenya Sheikh Hussen Shariff ametoa wito kwa Wakenya ambao wana nia ya kutekeleza ibada ya Hija na bado hawajapata pasi za kusafiria kuwasilisha maombi ya pasi hizo haraka iwezekanavyo ili waweze kupata visa kwa wakati.

Aidha Sheikh Shariff amesema visa ya Hija hivi sasa inapatikana kwa njia ya intaneti na kwamba Wakenya wanaweza kujaza fomu hizo na wakabidhiwe visa punde watakapowasili Saudia.

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha