IQNA

Maulamaa wa Ummah watoa fatwa kuhusu Kuyahudishwa Quds Tukufu

11:54 - June 07, 2009
Habari ID: 1788149
Maulamaa 52 Waislamu wametoa fatwa isemayo kuwa ‘ Ni haramu kupuuza haki za Waislamu wa Quds na Msikiti wa Al Aqsa. Vile vile wamesema kuanzisha uhusiano na Utawala wa Kizayuni ni haramu’.
Kwa mujibu wa tovuti ya attajdid.info, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina Raid Salah aliyeshiriki katika kongamano la ‘Mwaka 42 wa Kukaliwa Kwa Mabavu Quds na Msikiti wa Al Aqsa’ amesema matini ya fatwa hiyo ilitiwa saini na Maulamaa maarufu kama vile Sheikh Yusuf Qaradawi, Sheikh Salman bin Fahd al Audah na Maimamu wa Jamaa kutoka Saudi Arabia, Uturuki, Palestina, Mauritani na Jordan.
Fatwa hiyo inasema hivi: “Kuikomboa Quds Tukufu, Msikiti wa Al Aqsa na ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni wajibu wa Kisheria. Kila Muislamu anapaswa, kwa kuzingatia hali na uwezo wake’ kujitahidi kufanikisha lengo hili. Al Quds na Msikiti wa Al Aqsa ni majina yaliyotajwa katika matini za Quran na Hadithi za Mtume (SAW) na kuarifishwa kama maeneo matakatifu na hivyo hayapaswa kupuuzwa”. 417153
captcha