IQNA

Sala ya Idu

Sala za Idul Fitr yavutia umati mkubwa huko Karbala, Iraq

11:05 - April 11, 2024
Habari ID: 3478671
IQNA - Sala ya Idul Fitr katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq ilishuhudia mahudhurio makubwa ya waumini na wafanyaziyara siku ya Jumatano.

Sala ya Idul Fitr iliswaliwa katika makaburi mawili matukufu  ya Imam Hussein (AS) na Hadhrat Abbas pamoja na katika eneo linalojulikana kama Bain-ul-Haramain, eneo lililo kati ya makaburi hayo mawili matukufu.

Sheikh Ahmed al-Safi aliongoza sala na kutoa khutba katika eneo hilo takatifu, tovuti ya al-Kafeel iliripoti.

Katika khutba zake, Sheikh al-Safi amekosoa ukimya wa nchi na vyombo vya habari vya dunia kuhusu jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.

Vile vile ameukosoa Umoja wa Mataifa kwa kufanya lolote kusimamisha mauaji ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kurejesha haki za watu wa Palestina.

Hapo awali ofisi ya Ayatullah Ali al-Sistani, kiongozi mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, ilitangaza Jumatano kuwa Idul Fitr katika nchi hiyo ya Kiarabu.

 

4209810

Kishikizo: idul fitr iraq karbala
captcha