IQNA

Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za braille yatolewa katika misikiti ya Morocco

15:27 - August 15, 2010
Habari ID: 1973912
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imeanza kugawa nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za braille (makshsusi kwa wasioona) katika misikiti ya nchi hiyo kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Jumuiya ya Wasioona ya Morocco ikishirikiana na Wizara ya Wakfu ya nchi hiyo imechapisha nakala 62 elfu za Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za braille na zimeanza kugawanywa katika misiki ya nchi hiyo tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani.
Kwa kutilia maanani sifa makhsusi ya maandiko ya Qur'ani kwa hati za braille ambayo huchukua nafasi kubwa ikilinganishwa na hati za kawaida, kila nakala moja ya Qur'ani hizo za braille makhsusi kwa wasioona imechapishwa katika juzuu sita na kila juzuu ina hizbu 10.
Vilevile Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imetuma idadi kadhaa ya makari, watoa mawaida na maimamu wa misikiti katika nchi za Ulaya katika mwezi huu wa Ramadhani kwa shabaha ya kuwaongoza na kuwaelimisha Waislamu wa nchi hiyo wanaoishi huko na kuwalinda mbele ya mirengo potofu. 633709

captcha