IQNA

Mashia wa Ufaransa kuomboleza kifo cha Imam Hussein (as)

17:13 - December 05, 2010
Habari ID: 2042695
Mashia wanaoishi Paris mji mkuu wa Ufaransa wamepanga kukutana katika Jumuiya ya Beit az-Zahra (as) kuomboleza mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as) na wafuasi wake waaminifu.
Maombolezo hayo yataanza kufanyika siku ya Alkhamisi Disemba 9 mara tu baada ya kusimamishwa swala ya jamaa ya Isha na Maghrib na kusomwa dua ya Kumeil na ziara ya Ashura.
Maombolezo hayo yatakuwa yakifanyika kila siku hadi Jumatano tarehe 15 Disemba. Ratiba maalumu ya maombolezo ya Imam Hussein (as) imepangwa kutekelezwa siku ya Alkhamisi Disemba 16 ambapo maombolezo yataanza kufanyika asubuhi kuanzia saa tano. Katika siku hiyo waombolezaji watasoma Qur'ani Tukufu na ziara ya Ashura ya kuwakumbuka mashahidi wa Karbala.
Jumuiya ya Beit az-Zahra (as) imetoa taarifa ikiwawataka Mashia na wapenzi wa Ahlul Beit wa Mtume (saw) wahudhurie maombolezo hayo ili kuyafanikisha. 706556
captcha