IQNA

Kuongezwa hatua za usalama nchini siku ya Ashura

18:51 - December 08, 2010
Habari ID: 2044807
Askari wapatao 25,000 wamewekwa tayari kwa lengo la kutekeleza operesheni maalumu za kulinda amani katika siku ya Ashura mjini Karbala na katika maeneo mengine ya Iraq.
Huku ikitangaza habari hiyo polisi ya mjini Karbala imesema kuwa idadi hiyo ya walinda usalama imewekwa katika maeneo tofauti ya mji wa Karbala ili kudhamini usalama na utulivu wa waombolezaji katika siku hiyo.
Kila mwaka mamilioni ya waombolezaji kutoka kila pande za Iraq na katika nchi nyingine za ulimwengu hukusanyika katika haram ya Imam Hussein (as) mjini Karbala kwa lengo la kuomboleza kuuawa shahidi na kinyama mjukuu huyo wa Mtume Mtukufu (saw).
Katika miaka ya hivi karibuni magaidi wamekuwa wakiwalenga waombolezaji hao katika siku ya Ashura na kuwaua kigaidi. 708244
captcha