IQNA

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vyakwepa kutangaza maombolezo ya Ashura

12:58 - December 18, 2010
Habari ID: 2048800
Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimekwepa kutangaza na kuakisi kwa njia yoyote maombolezo ya Ashura ya kuuawa shahidi Imam Hussein (as) ambaye ni mjukuu wa Mtume Mtukufu (saw).
Vyombo hivyo vya habari vimechukua hatua hiyo katika hali ambayo Mashia zaidi ya milioni mbili wa nchi hiyo wameshiriki kwa wingi katika maombolezo hayo yaliyofanyika katika miji tofauti ya Saudi Arabia.
Mashia wa Saudi Arabia walikutana na kukusanyika kwa makumi ya maelfu katika misikiti na Husseiniya tofauti katika miji ya Ahsaa na Qatif kwa lengo kukumbuka na kuomboleza siku ya Ashura ambapo Imam Hussein (as) na wafuasi wake waaminifu 72 waliuwa kinyama na jeshi la dhalimu Yazid bin Muawiya katika ardhi ya Karbala nchini Iraq. Hii ni katika hali ambayo Ashura ni mnasaba wa pili kwa ukubwa baada ya hija kutekelezwa na Mashia wa Saudi Arabia ambapo zaidi ya watu milioni mbili hushiriki.
Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimepigwa marufuku rasmi na watawala wa nchi hiyo kuakisi maombolezo yoyote yanayohusiana na Ashura, na kana kwamba hilo halitoshi, vimezuiwa pia kuakisi kwa njia yoyote ile fikra za wasomi na wanafikra wa Kishia wa nchi hiyo.
Katika kudumisha siasa zao za kibaguzi dhidi ya Mashia, hakuna Shia yoyote anayeruhusiwa kisheria kumiliki au kuendesha chombo chochote cha habari nchini humo. 713318
captcha