IQNA

Marasimu ya Ashura kufanyika Finland

15:07 - December 04, 2011
Habari ID: 2233886
Marasimu ya Ashura ya Imam Hussein (as) yamepangwa kufanyika siku ya Jumanne Disemba 6 huko Helsinki mji mkuu wa Finland.
Marasimu hayo yatafanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Ahlul Beit (as). Kwa mujibu wa tovuti ya Swautul Iraq, marasimu hayo yataanza saa saba za adhuhuri ambapo idadi kubwa ya wapenzi na wafuasi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) inatazamiwa kushiriki.
Tayari kituo kilichotajwa kimetoa wito kwa waombolezaji na wafuasi wa Ahlul Beit (as) kushiriki kwa wingi katika maombolezo ya siku hiyo ya Ashura. Watayarishaji wa maombolezo hayo wamesema kwamba tayari wamekwishapokea kibali rasmi cha kuandaa maombolezo hayo kutoka kwa serikali ya Helsinki na kwamba msafara wa maombolezo unatazamiwa kuanzia katika majengo ya bunge hadi kwenye kituo cha treni ya chini kwa chini kwenye mji huo.
Kituo cha Kiislamu cha Helsinki kimewaalika wapigania haki na uadilifu wote pamoja na wafuasi wa Ahlul Beit kujiunga na maombolezo hayo ya adhuhuri ya Ashura ili kuwabainishia walimwengu ukweli na malengo halisi ya mapambano ya Imam Hussein (as) dhidi ya watawala dhalimu waliotaka kupotosha na kuutumia vibaya Uislamu kwa lengo la kudhamini maslahi yao binafsi ya kidunia. 910008
captcha