IQNA

11:44 - May 24, 2012
News ID: 2332990
Msikiti wa kwanza wa Waislamu wa madhehebu ya Shia umefunguliwa katika mji mkuu wa Finland, Helsinki.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA barani Ulaya, Msikiti huo pia utajumuisha kituo cha utamaduni. Sherehe za kufunguliwa msikiti huo uliopewa jina la Msikiti wa Fatima Zahra SA zilihudhuriwa na wanazuoni wa Kiislamu kutoka Sweden, Denmar na Norway wakiwemo Hujjatul Islam Hakim Elahi, Hujjatul Islam Khademi na Hujjatul Islam Razavi pamoja na Balozi wa Iran Finland Sayyed Rasoul Mousavi. Vile vile mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu wa Finland alihudhuria sherehe hivyo.
Msikiti huo umejengwa na Kituo cha Risalat Ahul Bayt AS ambacho kinafungamana na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS.
Kituo hicho kilianza shughuli zake nchini Finland miaka 10 iliyopita na kina wanachama 1000. Kituo hicho kinachapisha jarida la Kiislamu lijulikanalo kama Salam na kuchapisha vitabu vine vya Kiislamu kwa lugha ya Kifini.
Kituo hicho pia huandaa shughuli za kiutamaduni kwa ushirikiano na makanisa ya nchi hiyo.
1013768
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: