IQNA

Brazil yaruhusu Hijabu katika vitambulisho

5:05 - September 25, 2012
Habari ID: 2418906
Wanawake Waislamu nchini Brazil wataruhusiwa kuvaa vazi la Hijabu katika picha za vitambulisho vya kitaifa, pasipoti, leseni ya kuendesha gari n.k.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hatua ya imechukuliwa kitaifa baada ya kupitishwa kwanza katika jimbo la mpakani Foz do Iguaçu magharibi mwa nchi hiyo.
Mohsin Alhassani mkurugenzi wa Msikiti wa Omar ibn al Kattab huko Foz do Iguaçu amesema 'hijabu si nadharia, ni sehemu ya mavazi ya wajibu ya wanawake Waislamu.'
Hijabu iligeuka suala la kitaifa hivi karibuni Brazil baada ya mkaazi Mwislamu Ahlam Abdul El-Saifi kukataa kutoa vazi hilo la stara wakati akipigwa picha ya leseni ya kuendesha gari katika mji wa Sao Bernardo do Campo katika jimbo la Sao Paulo. Tukio sawa na hilo pia liliripotiwa katika mji wa Foz do Iguaçu. Baraza la mji huo lilisikiliza malalamiko ya Waislamu na kutuma pendekezo kwa serikali ya kitaifa likitaka wanawake Waislamu waruhusiwa kuvaa hijabu wakati wakipigwa picha za vitambulisho rasmi.
Uamuzi wa kuidhinisha Hijabu katika vitambulisho unatazmaiwa kuidhinishwa rasmi katika kipindi cha mwezi moja ujao.
Inakadiriwa kuwa Waislamu katika mji wa Foz do Iguaçu ni karibu elfu 20 kati ya wakaazi laki mbili na nusu. Idadi ya Waislamu Brazil inakadiriwa kuwa milioni moja na nusu.
1105561
captcha