IQNA

Imam Khamenei: Vijana Iran mstari wa mbele kukabiliana na maadui

11:49 - October 14, 2012
Habari ID: 2431115
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema kuwa, ‘kizazi cha vijana nchini Iran kiko katika mstari wa mbele kukabiliana na madola makubwa yanayojitakia makuu’.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo Jumamosi alasiri mkoani Khorassan Kaskazini katika eneo la kaskazini mashariki mwa Iran wakati alipokutana na familia za mashahidi, walemavu wa vita na watu waliojitolea katika kujihami kutakatifu.

Katika hotuba yake, Ayatullah Khamenei amesema moyo wa vijana wa Iran kusimama kidete na kupigania kujitegemea ni natija ya baraka ya damu ya mashahidi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema baadhi ya watu wameondoka katika mkondo wa mapinduzi kwa sababu ya uchovu, shaka au hadaa ya tabasamu ya maadui lakini mkabala wa hilo, kwa baraka ya damu ya mashahidi kizazi kipya cha vijana kina mbinu nyingi mpya jambo ambalo limeleta moyo wa kujitolea, uthabiti na izza kote Iran. Ameongeza kuwa leo kizazi cha vijana ambao hawakumuona Imam Khomeini MA wamesimama kidetea katika kukabiliana na madola yanayojitakia makuu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa la Iran linapaswa kuzishukuru familia za mashahidi na pia amewataka watoto wa mashahidi kuwa na fakhari kutokana na mirathi yenye thamani ya baba zao ambayo inapaswa kukabidhiwa vizazi vijavyo.
1118762
captcha