IQNA

Jeshi katili la Israel laua Wapalestina 17 Ukingo wa Magharibi, Guterres ataka mashambulizi yakomeshwe

16:01 - August 29, 2024
Habari ID: 3479347
IQNA-Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Israel usitishe mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukingo wa Magharibi ambayo yamepelekea Wapalestina wasiopungua 17 kuuawa shahidi.

Katika taarifa yake, Guterres ametoa wito wa "kukomeshwa mara moja" kwa uchokozi wa utawala dhalimu wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi yake dhidi ya maeneo ya Jenin, Tulkaram na Tubas.

Mapema siku ya Jumatano, jeshi katili la Israel ilitekelezwa operesheni yake kubwa zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 - iliyoitwa "Kambi za Majira ya Joto" - katika Ukingo wa Magharibi. Katika operesheni hiyo, jeshi katili la Israel limetekeleza mashambulizi ya nchi kavu na ya anga dhidi ya maeneo ya Wapalestina.

Takriban Wapalestina 17 wameuawa katika uvamizi na mashambulizi  hayo ya Israel katika miji kadhaa, huku wengine wengi wakijeruhiwa. Wanane kati yao wameuawa huko Jenin, watano Tulkaram na wanne Tubas.

Guterres amelaani vikali vifo vya watu wakiwemo watoto na kuutaka utawala wa Israel kuwalinda raia na kudhamini usalama wao.

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas alifupisha safari yake Saudi Arabia na kurejea Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatano kutokana na mashambulizi hayo ya utawala haramu wa Israel katika maeneo ya kaskazini mwa ardhi hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambao katika mahojiano siku ya Jumatatu, waziri mwenye misimamo mikali wa utawala wa Israel Itamar Ben-Gvir alitangaza mpango wa kujenga sinagogi la Kizayuni ndani ya Msikiti wa al-Aqsa katika eneo la Quds (Jerusalem) Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Tamko hilo limelaaniwa vikali kimataifa.

3489697

Habari zinazohusiana
captcha