IQNA

TEHRAN (IQNA) – Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewashambulia Wapalestina waliokuwa wakiandamana katika kijiji cha Beit Dajan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupinga ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni.

Waandamnaji kadhaa walijeruhiwa wakati askari wa Israel waliptumia risasi za plastini na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya. Ujenzi wa vitongoji hivyo ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.