IQNA – Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Umma nchini Uhispania (RTVE), José Pablo López, amemkemea Mkurugenzi wa Mashindano ya Muziki ya Eurovision kwa barua yake ya wazi kwa mashabiki ambayo haikutaja Gaza wala utawala wa Israel, akisema hatua hiyo ni “kushindwa” wakati mashindano hayo yanapitia mgogoro mkubwa wa kiheshima.
Habari ID: 3481653 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/13
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen, Abdul‑Malik al‑Houthi, amelaani vikali ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wanawake wa Palestina, akisema maelfu ya wanawake—akiwemo wajawazito, wasichana wadogo na wazee—wameuawa katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3481649 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/12
IQNA – Harakati ya mapambano ya Hizbullah nchini Lebanon imemtaka Kiongozi wa Kanisa Katoliki kulaani ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita na mashambulizi ya Israel dhidi ya taifa hilo la Kiarabu.
Habari ID: 3481592 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/30
IQNA – Makamu wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Hussein al-Sheikh, amesifu tamko la pamoja la Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza lililolaani kuongezeka kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi.
Habari ID: 3481581 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/28
Maoni
IQNA-Afisa wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel amefichua kuwa taarifa za kijasusi za Israel zilichochea mapigano ya Darfur, Sudan ili kuisukuma hali kuelekea kwenye mgogoro na mgawanyiko zaidi, na kwamba mapigano ya sasa nchini humo hatimaye yataishia kwa kugawanywa katika maeneo kadhaa.
Habari ID: 3481576 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/27
IQNA – Mufti Mkuu wa Oman ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na nchi za Kiislamu kuushinikiza utawala wa Kizayuni kusitisha ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481527 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/17
IQNA – Katika kura ya maamuzi yenye uzito, Shirikisho la Soka la Ireland (FAI) limeunga mkono azimio linaloitaka UEFA kuifukuza Israel kutoka kwenye mashindano ya kimataifa na ya vilabu barani Ulaya.
Habari ID: 3481491 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/09
IQNA – Mfungwa wa Kipalestina aliyeachiliwa kutoka gereza la utawala wa Kizayuni ameeleza mateso makali na hali isiyo ya kibinadamu inayowakumba wafungwa wa Kiislamu, ikiwemo udhalilishaji wa Qur'an Tukufu na kuzuia adhana na sala za jamaa.
Habari ID: 3481418 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/26
IQNA – Mamlaka za Palestina zimeonya kuwa shughuli za uchimbaji zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel karibu na Msikiti wa Al-Aqsa na katika Mji wa Kale wa Al-Quds (Jerusalem) zinaweza kuhatarisha uimara wa msikiti huo mtukufu.
Habari ID: 3481407 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/24
IQNA-Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) limetangaza kukabidhiwa mateka saba wa kwanza wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481361 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran
IQNA-Khatibu wa Swala ya Ijumaaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, miaka miwili baada ya Operesheni kubwa ya Kimbunga cha Al-Aqswa haiba ya utawala wa Kizayuni imejaa msukosuko na mparaganyiko.
Habari ID: 3481350 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/10
IQNA – Mamlaka ya utawala wa Kizayuni imezuia Sheikh Ikrima Sabri, khatibu wa Msikiti wa Al-Aqsa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la al-Quds (Jerusalem) kuingia na kuswali katika eneo hilo takatifu kwa muda wa miezi sita — hatua iliyolaaniwa vikali kama sehemu ya kampeni ya kuwalenga viongozi wa kidini wa Kipalestina.
Habari ID: 3481336 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/07
IQNA-Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, imesema iko tayari “kuwaachilia mateka wote Wa israel i, walio hai na waliokufa,” lakini imesisitiza kuwa hakuna utawala wa kigeni utakaoruhusiwa kusimamia Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481325 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/04
IQNA – Hatua ya utawala wa Israeli kuzuia meli za Msafara wa Kimataifa wa Sumud imezua shutuma kali kutoka kwa serikali na mashirika ya kimataifa kote duniani.
Habari ID: 3481315 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/02
IQNA-Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limesema ndege isiyo na rubani iliyorushwa kutoka Yemen imeshambulia mji wa kusini wa Eilat na kujeruhi watu 22 wakiwemo wawili ambao hali zao ni mahututi. Hayo yanajiri wakati jeshi la kizayuni likiwa lingali linaendeleza vita vyake vya kinyama na mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3481288 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/26
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mashambulizi ya anga ya “kikatili” yaliyofanywa na Marekani na Israel mwezi Juni katika ardhi ya Iran na kusema yalikuwa usaliti kwa diplomasia.
Habari ID: 3481282 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/25
IQNA – Polisi wa utawala wa Israel wamemkamata Sheikh Mohammad Sarandah, khatibu wa Msikiti wa Al-Aqsa, muda mfupi baada ya kutoa hotuba ya Ijumaa, kwa mujibu wa Waqfu wa Kiislamu wa al-Quds.
Habari ID: 3481258 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/20
IQNA – Video ya Tarteel ya Qur’an iliyosomwa na shahidi Hammam al-Hayya, mwana wa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Khalil al-Hayya, ambaye aliuawa shahidi hivi karibuni nchini Qatar, imesambazwa mtandaoni.
Habari ID: 3481244 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/16
IQNA – Kiongozi wa Harakati za Kiislamu nchini Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky, amesema kumeshuhudiwa ongezeko la mwamko na uungaji mkono kwa Wapalestina katika nchi za Magharibi.
Habari ID: 3481242 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/16
Taarifa ya Kikao cha Doha
IQNA – Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wamelaani vikali mashambulizi ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji mkuu wa Qatar, Doha, wakionya kuwa hatua hiyo inahatarisha amani ya kikanda na wakitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti.
Habari ID: 3481240 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/16