IQNA

TEHRAN (IQNA)- Taha Ezzat ni kijana mwenye umri wa miaka 17 kutoka mkoa wa El Beheira Misri na amepata umashuhuri Misri na duniania kutokana na qiraa yake ya Qur'ani Tukufu.

Ustadh Ezzat ni mwanafunzi katika moja ya taasisi za kidini za Al Azhar mkoani El Beheira na amekuwa akiendelea na masomo yake ya sekondari sambamba na kujifunza Qur'ani Tukufu. Baba yake Ezzat ni moja kati ya maimamu na mahatibu wa misikiti inayosimamiwa na Wizara ya Wakfu ya Misri.

Ezzat alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka sita na alipofika miaka 10 alikuwa amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Kijana huyu mwenye kipaji anasema anamuiga Sheikh Mahmoud Shahat Al Anwar katika qiraa yake ya Qur'ani.

Katika klipi hii Ustadh Ezzat anasoma aya za 31 hadi 36 za Surah Qaf katika Qur'ani Tukufu.

4015714/

کد ویدیو
Kishikizo: anwar ، qiraa ، qurani tukufu ، misri