IQNA

Makumbusho ya Qiraa ya Qur'ani yazinduliwa Caiaro ili kuhifadhi turathi ya sauti

15:14 - June 09, 2025
Habari ID: 3480812
IQNA – Makumbusho mapya yanayolenga kuhifadhi kumbukumbu adimu za Qiraa au usomaji wa Qur'ani wa maqari maarufu wa Misri yanatarajiwa kufunguliwa katika jengo la kihistoria la Maspero jijini Cairo, katika makao ya redio na televisheni ya taifa.

Makumbusho ya Qiraa ya Qur'ani ya Maspero yamekusudiwa kulinda hazina ya sauti za asili kutoka kwa baadhi ya maqari waliotia fora  katika historia ya Qur’ani katika karne moja iliyopita, wakiwemo Sheikh Muhammad Rifaat, Sheikh Mustafa Ismail, Sheikh Mahmoud Khalil Al-Husary, na Sheikh Abdul Basit Abdul Samad.

Kumbukumbu hizi, nyingi kati yake zikiwa za miongo kadhaa iliyopita, zimekuwa nguzo muhimu katika kuunda ladha ya usomaji wa Qur’ani katila ulimwengu wa Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.

Mradi huu umeibuka wakati ambapo kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI) katika kuunda sauti za binadamu, hasa katika muktadha wa kidini au wa kitamaduni.

Ingawa maudhui yaliyotengenezwa kwa AI yameanza kupata umaarufu, wengi wanaamini kuwa hayawezi kufikia uzito wa kiroho unaopatikana katika usomaji halisi wa kibinadamu. Katika muktadha huu, makumbusho haya yanaangaliwa kama hatua muhimu ya kuhifadhi asili halisi na nguvu ya kihisia ya sauti hizi za kihistoria.

Ahmed Al-Muslimani, mkuu wa Mamlaka ya Habari ya Taifa ya Misri, amethibitisha kuwa makumbusho haya yatakuwa wazi kwa wageni wa ndani ya Misri pamoja na wale wa kimataifa, hasa kutoka ulimwengu wa Kiislamu.

3493377

captcha